Clean Up: Dawa ya kuua magugu aina zote, nzuri kwa ajili ya kuandaa shamba

Clean UP ni dawa ya kuua magugu kiuagugu kisichochambua magugu ambayo tayari yamekwishachomoza ardhini

Clean UP ni dawa ya kuua magugu au kiuagugu kisichochambua magugu ambayo tayari yamekwishachomoza ardhini.

Clean UP inafyonzwa kupitia sehemu za kijani za mimea na inaua magugu kwa kuharibu mfumo wa uzalishaji wa protini. Clean UP ina ufanisi wa hali ya juu kudhibiti magugu sumbufu yaliyo na usugu kwenye viuagugu vingine.

Kama umevutiwa na dawa ya Clean Up, bofy kitufe cha WhatsApp Message au Pga simu kuwasiliana nasi.


Clean Up ni Kiuagugu Kisichochagua magugu. Clean Up 48 SL ina Glyphosate isopropylamine salt 480g/Lt. Inatumika kuandaa shamba.

Clean Up ni kiuagugu kinachodhibiti magugu sugu ya msimu na yale yaotayo mwaka mzima kwenye mazao ya aina mbalimbali. Clean UP inaweza kutumika kuandaa shamba kabla ya kupanda au baada ya kupanda kwa ajili ya palizi kwa kufuata maelekezo maalum.

Maelezo ya Matumizi

Hakiki bomba lako kwa ufasaha kabla ya kunyunyiza. Tikisa kiatilifu chako vizuri kabla ya kuchanganya na maji. Weka maji kidogo kwenye bomba, kisha ongezea kiasi cha Clean Up kinachoshauriwa tikisa kwa kuzungusha huku ukiendelea kujaza maji kufikia kiasi kinachohitajika. Osha kipimio chako kwa maji safi mara tatu na mimina maji uliyooshea kwenye bomba. Kifungashio kitupwe kwa kufuata sharia na ikibaki funga kwa kukaza vizuri.

Maelezo ya Kitaalamu

Ili kupata matokeo mazuri hakikisha magugu yamechoza, kuna unyevu shambani na magugu yanaendelea kustawi. Magugu yatakayochomoza kutoka kwenye mbegu au kwenye mizizi iliyokuwa ardhini baada ya kutumia kiua gugu hiki hayatazuiwa, hivyo hakikisha magugu yote yawe yamechomoza.

Magugu yanayodhibitiwaMl/20L
Magugu ya msimu na mwaka150-200
Magugu yaotayo kwa mwaka mara mbili au zaidi300
Udhibiti wa visiki vinavyoota upya na udhibiti wa magugu pori kwenuye miwa400-600
Matumizi: Clean Up

NB: Tumia maji safi, sio yenye tope.

Muda salama wa kuingia: Angalau siku 3.

Muingiliano

Kuchanganya na viuagugu vingine itapunguza ufanisi wa Clean Up, lakini unaweza kuchanganya na viuatilifu vyenye Atrazine + Metolachlor.

Jinsi ya Kujilinda

• Usivute mvuke au moshi wake wakati kunyunyiza
• Isiguse macho, ngozi na nguo
• Vaa mavazi na vifaa vya kujikinga kama glovu na kinga macho na usichanganye bila kujikinga vizuri
• Usile, usinywe na kuvuta sigara kipindi utumiapo.
• Hakikisha unaoga baada ya kunyunyiza na badilisha nguo
• Safisha vifaa vilivyotumika na mikono kwa maji mengi masafi

Tahadhari ya Uhifadhi

• Usihifadhi karibu na chakula, maji, vyakula vya mifugo. Hifadhi sehemu kavu na yenye hewa ya kutosha. Utupaji wa vifungashio
• Vifungashio vitupwe sehemu maalumu iliyoidhinishwa na wasimamizi wa viuatilifu, zingatia sheria za mazingira za nchi husika.

Huduma ya kwanza

• Ikigusa ngozi. Nawa maji mengi na sabuni kisha toa nguo zilizochafuka.
• Ikigusa macho, osha macho kwa maji mengi kwa muda wa dakika 15 kisha muone daktari.
• Ikimezwa, usimtapishe wasiliana na mtabibu au mpeleke mwathirika kwenye huduma ya dharura hospitali, haina makata sumu tibu kutokana na dalili.
• Ikivutwa, mtoe mwathirika mpeleke sehemu yenye hewa ya kutosha na apate huduma ya kiafya kama mwathirika anashindwa kuhema.
• Kwa dharura. Wasiliana na kituo cha kuzuia sumu kwa ushauri.

Kufahamu zaidi kuhusu Clean Up, bofya moja ya vitufe vifuatavyo kuwasiliana nasi moja kwa moja.

Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    Call Us Now...!