Maswali yanayoulizwa mara nyingi kuhusu Kampuni na bidhaa

📝BareFoot International Limited ni nini❓

BareFoot International ni kampuni ya kilimo biashara iliyosajiliwa Tanzania kwa lengo la kufanya biashara ya uuzaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo ikiwemo mbolea, mbegu, madawa na zana pamoja na mashine. Kampuni ya Barefoot International limited inafanya kazi Tanzania nzima kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita Iringa Kagera, Katavi, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Mjini Magharibi, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Pemba Kaskazini, Pemba Kusini, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora, Tanga, Unguja Kaskazini na Unguja Kusini.


📝Mnatoa huduma na bidhaa gani❓

Kampuni ya Barefoot International limited inauza bidhaa mbalimbali zikiwemo mbolea (Master Grower na Master fruiter), Dawa ya kudhibiti kuvu na ukungu (Master kutu), Viuagugu au dawa za kuulia magugu (Clean Up), Viuadudu au dawa za kuulia wadudu (Indomectin), mbegu za mazao (mboga mboga), zana na mashine (Mabomba ya kupulizia sumu).


📝Kwa nini nitumie bidhaa zenu❓

✅ Tunahakikisha kuwa tunasambaza na kuuza bidhaa zenye ubora na utendaji wa hali ya juu. Tumia bidhaa zetu kwa sababu zina ubora wa hali ya juu uliopimwa na kuthibitishwa. Vilevile, tunahifadhi bidhaa zetu kwa namna bora ili kuhakikisha ubora wa bidhaa zetu haupungui.


📝Nawezaje kutumia bidhaa zenu❓

✅Kufahamu kuhusu jinsi ya kutumia bidhaa zetu, soma na kufuata maelekezo kwenye lebo ya bidhaa husika au karatasi inayoambatanishwa na bidhaa husika.


📝Mimi ni mkulima. Nawezaje kupata bidhaa zenu❓

✅Kama wewe ni mkulima unaweza kupata bidhaa zetu kupitia maduka ya pembejeo nchi nzima. Tunasambaza bidhaa zetu karibu maduka yote ya pembejeo Tanzania. Kama utashindwa kupata bidhaa unayoitaka katika maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo karibu na wewe, usisite kuwasiliana nasi.


📝Mimi ni muuzaji wa pembejeo za kilimo na mifugo. Nawezaje kupata bidhaa zenu

✅Kama wewe ni muuzaji wa pembejeo za kilimo na mifugo, unaweza kupata bidhaa zetu kupitia wawakilishi wetu walioko karibu na wewe. Tunao wawakilishi mikoa yote Tanzania, watakuunganisha nasi na utaweza kununua na kuuza bidhaa zetu. Kama unatamani kufanya biashara nasi unakaribishwa sana, usisite kuwasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    Call Us Now...!