Dawa nzuri ya kuua magugu na kuandalia mashamba

Kampuni ya Barefoot International Limited inauza dawa ya kuulia magugu yenye Glyphosate inayoitwa Clean Up.

Glyphosate ni aina ya dawa ya kuua magugu ambayo inayoua aina zote za magugu bila kuchagua aina ya majani. Ni dawa ya kuulia magugu inayotumika sana duniani. Dawa hii inaua magugu yenye majani ya aina zote yaani majani mapana na membamba. Dawa hii inapigwa tuu wakati wa kuandaa shamba, haipigwi kwenye mazao kwa sababu inaweza kukausha mazao.

Clean Up inanyonywa kupitia majani na kusafirishwa kwenye mmea unaoota. Kwa sababu hiyo, hufanya kazi vizuri kwenye magugu ambayo yameanza kuota na haiathiri mimea ambayo haijaota.

Mambo ya Kuzingatia

Utendaji wa Clean Up unaathiriwa na mambo mengi kama; uchanganyaji wa dawa nyingine wakati wa kupiga, Kiasi cha dawa unachopiga, kiasi cha maji, usafi wa maji na muda dawa hii inapopigwa. Zingatia mambo haya kabla ya kutumia dawa hii.

Vilevile, mambo yote yanayoathiri ukuaji wa mimea yanaweza kuathiri utendaji wa Clean Up. Kwa mfano, dawa hii ikipigwa kipindi cha ukame inaweza isifanye kazi vizuri. Dawa hii inafanya kazi vizuri wakati magugu yanastawi vizuri.

Unaweza kuongeza kiasi cha dawa kulingana na aina ya magugu na ukomavu wake. Unaweza usione matokeo mazuri ya dawa hii kama usipozingatia kipimo kulingana na aina ya magugu.

Clean Up: Dawa ya kuua magugu aina zote, nzuri kwa ajili ya kuandaa shamba

Clean Up ina ufanisi wa hali ya juu kutibu magugu sugu yaliyo na usugu kwenye viuagugu vingine.

Inadhibiti magugu sugu ya msimu na yale yaotayo mwaka mzima kwenye mazao ya aina mbalimbali...
Shopping Cart
0
    0
    Your Cart
    Your cart is emptyReturn to Shop
    Call Us Now...!