Kuhusu Kampuni ya BareFoot International Limited

Kuhusu Kampuni

Wasambazaji wa Pembejeo za Kilimo na Mifugo

Kampuni ya BareFoot International ni kampuni ya kilimo biashara iliyosajiliwa Tanzania kwa lengo la kufanya biashara ya pembejeo za kilimo na mifugo kama vile mbolea, mbegu, dawa za kilimo na mifugo pamoja na zana na mashine. Namba ya usajili ni 128811, 2016.

Historia ya Kampuni

Kampuni ilianza kufanya kazi Septemba 2016 kama msambazaji wa pembejeo za kilimo kwa zaidi ya mikoa 18 ya Tanzania. Kwa wakati huo ilikua na ofisi kuu Arusha, mwaka mmoja baadae, kampuni ilijenga uaminifu kwa wateja wake wa ndani na nje ya nchi pamoja na makampuni yanayohusika na usambazaji wa pembejeo. Kwa sababu hiyo kampuni iliamua kuongeza wigo wa kazi zake.

Kwa sasa kampuni ina matawi manne yaliyopo Arusha, Mbeya, Mwanza and Morogoro. Ofisi kuu za kampuni zipo Arusha SunFlag, Unga Limited, Viwandani.

Kampuni inavyofanya kazi

Kampuni inasambaza bidhaa za pembejeo za kilimo na mifugo kwenye mikoa mikuu inayojihusisha na kilimo ikiwemo, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Shinyanga, Simiyu, Katavi, Sumbawanga, Rukwa, Tabora, Geita, Iringa, Njombe, Kagera and Tanga.

Kupitia muundo na mpangilio wake, kampuni imeweza kutengeneza mtandao wa wateja wa kudumu zaidi ya 2000 nchi nzima. Wateja hao ni maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo, makundi ya wakulima, vyama vya msingi, wakulima wakubwa na wasambazaji wengine wa pembejeo

Huduma na bidhaa zetu

Kampuni ya BareFoot international limited inajihusisha na uingizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo. Hii inajumuisha bidhaa za kilimo na mifugo ikiwemo zana na mashine.

Ofisi na Matawi

Ofisi yetu kuu ipo Arusha na Ofisi nyingine ndogo zipo Mbeya, Mwanza na Morogoro

Shopping Cart
Call Us Now...!