Ili Kabiliana na wadudu shambani unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo;
Boresha Aya ya mimea
Ni lazima kuimarisha rutuba kwenye udongo ili mimea iwe na afya. Mimea yenye afya ina uwezo wa kukabiliana na wadudu. Unaweza kutumia mbolea ili kuongeza rutuba kwenye udongo wako. Unaweza kutumia booster/busta zetu kuboresha afya ya mazao yako, Haster Mbolea ya Master Grower na Mbolea ya Master Fruiter.
Wanyama na wadudu wanaokula wadudu waharibifu
Unaweza kuzuia wadudu kwenye mazao yako kwa kuhifadhi makazi ya wanyama wanaokula wadudu waharibifu. Pamoja na wadudu wanaokula wadudu waharibifu
Kutumia dawa za kuua wadudu
Nyunyizia dawa za kuulia wadudu mapema asubuhi au jioni. Hii itaongeza ufanisi wa dawa. Unaweza kutumia dawa yetu ya kuua wadudu inayoitwa Indomectin. Soma zaidi kuhusu dawa hii hapa.
Kuchanganya mazao shambani
Panda mazao ya aina mbalimbali shambani. Hii ni njia nzuri ya kufanya wanyama wanaowinda wadudu wawepo kwa muda mrefu. Kwa mfano vinyonga.
Kulima kwa kubadili aina ya mazao
Unaweza kukabiliana na wadudu waharibifu shambani kwa kulima kwa kubadilisha aina ya mazao kila msimu au kila mpando. Hii itasaidia kupunguza wadudu wanaoshambulia aina moja ya zao kwa sababu zao husika halitakuwepo shambani.