Aina nzuri za Mbolea ya Kunyunyiza
Zifuatazo ni aina nzuri za mbolea ya kunyunyiza
Mbolea ya Master Grower
Mbolea ya Master grower ni mbolea maalumu kwa ajili ya kukuzia.
Mbolea hii inasaidia kukua kwa mimea na kuongeza ubora na wingi wa mazao yako.
Master Grower ni mbolea (booster/busta) yenye potassium, phosphorus na kiwango kikubwa cha Nitrogeni katika uwiano wa N:P:K 30:10:10. Master Grower inachochea ukuaji wa mimea, inaboresha ubora wa mazao na kuongeza mavuno.
Mbolea ya Master Fruiter
Mbolea ya Master Fruiter inasaidia kuongeza wingi wa matunda na maua pamoja na kuongeza ubora na wingi wa mazao ya matunda na maua.
Mbolea hii inapunguza kuanguka kwa maua na matunda.
Master Fruiter ni mbolea (booster/busta) yenye nitrogen, phosphorus na kiwangokikubwa cha potassium katika uwiano wa N:P:K 10:10:40. Master Fruiter inachochea ukuaji wa maua na matunda na kuongeza ubora wa mazao.
Jinsi ya kunyunyiza Mbolea inavyotakiwa
Ili upate matokeo mazuri wakati wa kunyunyiza mbolea ya maji unatakiwa kufuata vigezo vifuatavyo:
Chagua Mbolea Nzuri
Tumia mbolea nzuri yenye ubora na iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea. Tunapendekeza utumie mbolea ya Master Grower au Mbolea ya Master Fruiter kulingana na uhitaji wako.
Tingisha kabla ya Kunyunyiza
Unatakiwa kutingisha vizuri mbolea yako ya maji kabla ya kunyunyiza. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
Nyunyiza wakati hakuna upepo
Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
Nyunyiza asubuhi au jioni
Unatakiwa kunyunyizia mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.