Mbegu bora za bamia na jinsi ya kulima ili kupata faida
Mbegu bora za bamia na jinsi ya kulima ili kupata faida Read More »
Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine. Bamia huliwa kama matunda au hupikwa kama mboga pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine.
Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja. Nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa aina ya bamia zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.
Kama unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini kulingana na hali ya hewa ya eneo husika
Hakikisha shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza ili kuongeza uzaaji wa bamia.
Wadudu wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na
utitiri mwekundu. Dhibiti wadudu hawa kwa kufuata njia zinazopendekezwa na wataalamu wa kilimo Kwenye eneo lako.
Bamia hushambuliwa na magonjwa kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo eneo ulipo.